
Mwanaume mmoja aliwatongoza wanawake
watatu tofauti na nia yake ni kufanya upembuzi yakinifu ili mmoja wao
awe mkewe. Hivyo jamaa aliamua kuwapa jaribio kwa kuwapa Tsh. 500,000/=
kila mmoja huku akitaka kujua ni namna gani watazitumia.Mwanamke wa
kwanza alitumia pesa yote kununua vipodozi. Alitembelea duka la vipodozi
na urembo akajikwatua sawa sawa! Alivyorudi kwa mchumba wake
akamwambia,"nimeamua kutumia pesa yote kwa ajili ya kujipamba ili nizidi
kukupendezamachoni pako na kukuvutia maana nakupenda sana."Hakika yule
mwanaume akapendezwa sana na mpenzi wake.Mwanamke wa pili alinunua
zawadi kwa ajili ya bwana wake. Alinunua simu janja mpya kwa ajili ya
bwana wake, saa ya kisasa, nguo na viatu vizuri. Alivyofika kwa bwana
wake alimwambia,"pesa yote nimeitumia kununua hizi zawadi zako maana
nina kupenda sana."Jamaa akafarijika sanaMwanamke wa tatu aliwekeza zile
pesa kwenye soko la hisa na baada ya muda fulani alipata faida ya
shilingi 2,000,000/=. Mwanamke yule aliamua kumrudishia bwana wake ile
pesa aliyokuwa amepewa yaani laki 5 na pesa iliyokuwa imebakia alifungua
akaunti ya pamoja na bwana wake. Kisha yule mwanamke akamwambia yule
jamaa,"nahitaji kuwekeza na kuhifadhi kesho yetu kwa sababu nakupenda
sana."Hakika yule mwanamke alimfurahisha sana jamaa.Jamaa akatafakari
sana yale ambayo yalikuwa yamefanywa na wale wanawake baada ya kupewa
laki 5. Lakini mwisho wa siku jamaa aliamua kumwoa mwanamke wa kwanza
kwasababu anamakalio makubwa! Wanaume watabakia kuwa wanaume tu
0 maoni:
Post a Comment