Siku zote dunia ni HADAA ulimwengu SHUJAA,usemi huu mimi naukubali sana maana unazungumzia matendo kibao ambayo yanamfanya mwanaadam kuishi kwa aman kisha kuja kuishi kwa mateso yaani bila ya AMANI.
Hasa katika karne ya sasa vijana wengi sana hupenda kutanguliza kauli ya kusema "NITAFANYA KESHO" Hili ndilo kubwa zaidi kwa VIJANA wa siku hizi bila kujali kuwa HAKUNA ALIYEIYONA KESHO na ndio maana maendeleo huwa machache saana kwa VIJANA.
JE UNAWEZA KUJIMUDU VIPI KAMA KIJANA KATIKA MAENDELEO?
Katika maendeleo panahitajika mambo mengi saana ya muhimu ya kuyafanya na kuyaacha mambo ambayo yanayoweza kuku potezea muda hasa katika kutafuta maendeleo. na ndio maana kuna msemo unasema KUNA MUDA WA FURAHA NA KUNA MUDA WA HUZUNI. Lakini vijana wengi sana hukumbuka sana STAREHE kuliko maendeleo kwaajili hiyo ndo unakuta vijana wanabaki kukaa chini na kuanza kujijutia kuwa kwanini walicheza wakati walipo kuwa wanaingiza pesa? na kwanini hajapata maendeleo na mpaka anazeeka amezeeka akiwa masikini haya yote ni maswali ya watu waliochezea maendeleo katika maisha yao. je utajimudu vipi kama kijana katika kuendeleza maendeleo yako?
1. MATUMIZI YA OVYO
Matumizi kwa vijana ndio tatizo kubwa ambalo linasababisha kughalimu ukosaji wa maendeleo ya vijana katika jamii, na hili ndo suala muhimu sana kulifahamu kwa kila mmoja ambaye anayejiona kuwa anamatatizo ya kuto kukaa na pesa ndani ya nyumba au mfukoni ni lazima utambuwe kiasi au kima ambacho kitakuwa kinamfaa katika mahitaji yake ya siku mzima kuliko kutumia pesa ovyo bila manufaa yoyote.kwahiyo inatupasa kuangalia matumizi yetu
Itaendelea.................................................
BLOGU YA LEWIS MBONDE BLOG YASITISHA KUTOA MAUDHUI MTANDAONI
-
Kutokana na matakwa ya kisheria ya maudhiu ya kutoa huduma za kimtandao
bila kuwa na leseni iliyotolewa na mamlaka ya udhibiti wa huduma za
mawasiliano t...
8 years ago






0 maoni:
Post a Comment